Awamu ya 10 ya tuzo za AFRIMMA iliandaliwa huko Dallas Texas nchini Marekani Septemba 17 ambapo mwanamuziki wa Kenya Nadia Mukami alishinda tuzo.
Aliibuka kidedea katika kitengo cha mwanamuziki bora wa kike Afrika Mashariki. Alikuwa akipambana na wengine kama Nikita Kering na Fena Gitu wa Kenya, Maua Sama, Zuchu na Nandy wa Tanzania, Azawi na Spice Diana wa Uganda na Hewan Gebrewold wa Ethiopia.
Mwaka jana Zuchu ndiye alishinda katika kitengo hicho
Nadia alihudhuria hafla ya kutuza washindi wa AFRIMMA mwaka 2023 ambapo alishukuru waandalizi kwa tuzo hiyo.
Hafla hiyo, ilitumiwa pia kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka 2013.