Mwanamuziki wa Marekani Kanye West ameendeleza mzozo kati yake na mama ya watoto wake Kim Kardashian mitandaoni, kutokana na hatua yake ya kutumia sauti ya binti yao North West kwenye wimbo.
Kanye alimrushia Kim maneno kupitia mtandao wa X kwenye machapisho kadhaa ambayo baadaye alifuta. Alionekana kuzungumzia htua ya mwanamuziki Playboi Carti, ya kuomba Kim amruhusu amhusishe binti yao North katika wimbo.
Carti aliwasilisha ombi hilo baada ya Kim kuchapisha baadhi ya maneno ya wimbo wake uitwao “Fine Shit” ambapo ametaja nembo yake ya mavazi ya Skims.
Kim alisambaza ombi la Carti kwenye Insta Stories na inaonekana kwamba Ye alidhania kwamba ameridhia ombi la Carti la kuhusisha North kwenye wimbo.
Siku chache zilizopita, Ye alimshambulia Kim Kardashian kwa kujaribu kuzuia uzinduzi wa wimbo wake “Lonely Roads Still Go to Sunshine” ambao amemhusisha binti yao wa umei wa miaka 11 North na Sean “Diddy” Combs.
Kanye anasema anahisi kwamba Kardashian anawasimamia kwa njia isiyofaa watoto wao wanne na kumlaumu kwa kuwa ndumakuwili kwa kumkasirikia kwa kuweka sauti ya North kwenye wimbo huku akiridhia ombi la Playboi Carti.
Kim alikuwa ametishia kwenda mahakamani kutafuta apatiwe haki zote za kukaa na watoto wao wanne kwa sababu North alihusishwa kwenye wimbo na babake bila idhini yake.