Mwilu ataka mahakama kulinda wanawake na watoto

Martin Mwanje
1 Min Read
Philomena Mwilu - Naibu Jaji Mkuu

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ametoa wito kwa majaji wa Mahakama Kuu kuboresha dhamira yao ya kulinda wanawake na watoto walio hatarini.

Amesema hilo linaweza kufikiwa kupitia hatua zinazochukuliwa na idara ya mahakama zilizojikita kwa ushughulikiaji wa visa vinavyoripotiwa kwa misingi ya kibinadamu na kikatiba.

Mwilu ambaye pia ni Makamu Rais wa Mahakama ya Juu aliyasema hayo leo Jumatatu alipohutubia Mkutano wa Viongozi wa Mahakama Kuu uliofanyika mjini Naivasha.

Alisisitiza umuhimu mkubwa wa Mahakama Kuu kuendeleza maono ya kikatiba ya nchi na kuhakikisha upatikanaji wa haki wenye tija.

Akiangazia maudhui ya mkutano huo, “Kulinda Wanawake na Watoto walio Hatarini: Kuimarisha Uingiliaji wa Idara ya Mahakama kwa Upatikanaji wa Haki,” Mwilu alitaja hilo kuwa jambo la dharura na muhimu.

Alisema Mahakama Kuu, kama mhimili mkuu wa mfumo wa idara ya mahakama nchini, hutekeleza wajibu muhimu katika kuongoza utamaduni wa kikatiba kwa kulinda haki, kutekeleza uwajibikaji, na kuangazia maisha ya kweli ya raia.

Hususan, alielezea wasiwasi unaoonezeka juu ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia, ikiwa ni pamoja na mauaji ya wanake na kutaka mwitikio ulioratibiwa unaohusishha wadau mbalimbali ili kukabiliana na uovu huo.

 

Share This Article