Mwili wa Odira Nwobu kuzikwa mwezi ujao

Nwobu aliaga dunia Novemba mwaka jana akiwa katika ziara nchini Afrika Kusini.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwili wa mwigizaji wa Nigeria Odira Nwobu utazikwa mwezi ujao miezi kadhaa tangu alipoaga dunia akiwa nchini Afrika Kusini, haya ni kulingana na familia yake.

Alikuwa amekwenda kuzuru taifa la Afrika Kusini akiwa na marafiki mwezi Novemba mwaka 2025, alipokumbana na mauti katika njia tatanishi.

Mwandaaji wa filamu za Nollywood Stanley Ontop alichapisha bango la maelezo kuhusu mipango ya mazishi ya mwigizaji huyo aliyefariki akiwa na umri wa miaka 43.

Mipango ya mazishi ya Nwobu inaanza Ijumaa Aprili 10, 2026 saa kumi jioni na kesha itakayohusisha nyimbo, nyumbani kwa babake.

Kesho yake Jumamosi tarehe 11, mipango itaanza saa 1 asubuhi na kuchukuliwa kwa mwili wa msanii huyo kutoka makafani na kulazwa katika makazi ya babake kwa ajili ya kuuaga.

Mkutano wa mazishi utaanza saa nne asubuhi siku hiyo hiyo na kuendelea hadi jioni wakati ambapo mwili wa Nwobu utazikwa.

Jumapili Aprili 12, 2026, kutaandaliwa ibada ya shukrani katika kanisa la kianglikana la Mtakatifu Paulo, Umuenechi, jijini Awka, Jimbo la Anambra, Kusini Mashariki mwa Nigeria.

Share This Article