Mwigizaji Sarah Hassan azinduliwa balozi wa Dettol

Dismas Otuke
1 Min Read
L-R Management Trainee Mumo Muia , Assistant Brand Manager Hygiene Brenda Mokaya , Sarah Hassan, Country Manager Kenya Asif M Hashimi, Assistant Brand Manager OTC and Durex Eva Mugo, Senior Brand Manager Dettol Margaret Ngea

Mwigizaji Saraha Hassan ametangazwa kuwa balozi wa bidhaa za usafi za Dettol, maarufu kama Dettol Skincare.

Mwingizaji huyo ambaye ameshinda tuzo kadhaa zikiwemo mwigizaji bora wa kike wa runinga kwenye tuzo za Kalasha mwezi uliopita,amepata umaarufu katika tasnia ya filamu nchini.

Sarah ameiigiza katika vipindi kadhaa vya runinga vikiwemo Tahidi High, Zari,Just In Time,na Crime and Justice.

Bidhaa mpya ya Dettol Skincare soap with 2X moisturizers ni laini kwa ngozi na inaaminika kuondoa asilimia 99.9 ya bacteria.

“Nimetumia sabuni ya dettol tangu nikiwa mtito ; ni nzuri sana kwangu: Dettol ni bidhaa bora na nitajitahidi kukuza ueneaji wake,”akasema Sarah

“Sarah Hassan anajiunga na Dettol Skincare family na ni ushuhuda tosha kuwa atatusaidia kuafikia ajenda yetu” akasema Asif Hashimi, Meneja wa Reckitt Kenya

Share This Article