Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu nchini, KNCHR Roseline Odede ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kifo chake kimetangazwa na Naibu wake Raymond Nyeris, ambaye kwenye taarifa amesema kuwa Odede alifariki jana Ijumaa.
Nyeris ametaja kifo hicho kuwa pigo kubwa kwa tume hiyo.
Mrehemu Odede alikuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na pia awali alihudumu kama naibu mwenyekiti wa bodi ya kuwapiga msasa majaji na mahakimu.
Alikuwa wakili kwa zaidi ya miaka 30.