Mwandalizi wa fainali za AFCON 2025 na 2027 kubainika Septemba 27

Dismas Otuke
1 Min Read

Kamati kuu ya shirirkisho la kandanda barani Afrika CAF, linatarajiwa kutangaza mataifa yatakayoandaa fainali za kombe la Afrika mwaka 2025 na 2027.

Kamati hiyo ya CAF ilikutana jijini Cairo kujadili maendeleo ya mashindano mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Ivory Coast mwakani,makala ya kwanza ya mashindano ya ligi kuu ya Afrika.

Kulingana na Rais wa CAF Dkt.Patrice Motsepe,kamati hiyo itakutana tena Septemba 27 kutangaza mataifa yaliyopokezwa maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025 na 2027.

Waaniaji wa maandalizi ya fainali za mwaka 2025 ni Morocco,Algeria,Zambia na ombi la pamoja kutoka kwa Nigeria na Benin.

Algeria pia inawania kuandaa kipute cha mwaka 20027 pamoja na Misri na ombi la pamoja la Tanzania, Kenya na Uganda.

Website |  + posts
Share This Article