Mwanawe Gavana Orengo afunga pingu za maisha

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanawe Gavana wa Siaya James Oreng’o ,Michael alifunga pingu za maisha katika harusi ya kufana iliyoandaliwa Jumamosi katika kanisa la All Saints Cathederal kaunti ya Nairobi.

Michael alifanya harusi na mchumba wake wa muda mrefu Samantha Luseno.

Gavana Orengo waliohudhuria harusi hiyo na mkewe Betty Murungi, walifaharikia sherehe hiyo na hatua waliyopiga mwanao.

Viongozi wa matabaka mbalimbali walihudhuria harusi hiyo akiwemo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka.

Share This Article