Mwanasiasa wa Afrika Kusini Julius Malema afungwa miaka 5 gerezani

Iwapo mahakama itashikilia kifungo hicho,  Malema atapigwa marufuku kuwa mbunge kwa muda wa miaka mitano.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanasiasa wa Afrika Kusini Julius Malema. Picha/Hisani.

Mwanasiasa wa chama cha Economic Freedom Fighters nchini Afrika Kusini Julius Malema, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani.

Hakimu Twanet Oliver wa mahakama ya East London nchini humo, alisema mwanasiasa huyo alikabiliwa na mashtaka matano.

Mnamo mwaka 2025, kiongozi huyo mwenye miaka 45, alipatikana na hatia ya kufyetua risasi, matumizi mabaya ya bunduki katika eneo la umma na kuhatarisha maisha ya watu.

Hata hivyo mawakili wa mwanasiasa huyo walikata rufaa mara moja na kusababisha Malema kuachiliwa kwa dhamana huku kesi hiyo ikiendelea kusikizwa.

Iwapo mahakama itashikilia kifungo hicho,  Malema atapigwa marufuku kuwa mbunge kwa muda wa miaka mitano.

Huku akijitetea katika mji wa KuGompo  ambalo ni jina jipya la East London, Malema aliambia mahakama hiyo kwamba alifyetua risasi hewani alipokuwa akisherehekea.

Share This Article