Mwanariadha Pistorius aachiliwa huru baada kufungwa kwa miaka 9

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ameachiliwa huru, baada ya kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka kumi gerezani.

Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka 13 mwaka 2016, baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 14, 2013.

Mwanariadha huyo ambaye ni mshindi wa medali kadhaa za Olimpiki, alikuwa ametumikia kifungo cha miaka 9 kati ya 13 na ameachiliwa mapema Ijumaa kwa msamaha.

Pistorius, aliye na umri wa miaka 37, aliwekwa kwa kifungo cha nyumbani mwaka 2015 hadi 2016.

Hata hivyo, inaaminika kuwa mwanariadha huyo atasalia chini ya ulinzi mkali na kifungo cha nje hadi atakapokamilisha hukumu yake mwaka 2029.

Baadhi ya vikwazo alivyowekewa Pistorius ni pamoja na kutozungumza na vyombo vya habari, kutosafiri nje ya wilaya yake na kutumikia jamii.

Share This Article