Mwanariadha Kelvin Kiptum kuzikwa Ijumaa

Tom Mathinji
1 Min Read

Mazishi ya marehemu mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za marathoni Kelvin Kiptum sasa yatafanyika keshokutwa Ijumaa.

Mazishi hayo awali yalipangwa na familia yake kuandaliwa siku ya Jumamosi.

Rais William Ruto anatarajiwa kuyahudhuria.

Serikali imechukuwa jukumu la kupanga mazishi hayo na itayagharimia.

Wiki iliyopita, Rais Ruto alidhihirisha kujitolea kwake kuheshimu urathi wa Kiptum kwa kupeleka kundi la wahandisi kutathmini na kuangazia ujenzi wa nyumba yake.

Ujenzi huo unatekelezwa na kampuni ya Vaghjiyani Enterprises katika shamba la ekari nne huko Naiberi, na ujenzi huo uliingia siku ya nne jana Jumanne.

Kampuni hiyo pia inajenga nyumba nyingine ya wazazi wake katika kijiji cha Chepsamo.

Nyumba hiyo inatarajiwa kukamilika kesho Alhamisi kabla ya kukabidhiwa familia.

TAGGED:
Share This Article