Mwanamuziki wa Tanzania Zena Yusuf Mohamed maarufu kama Shilole au Shishi Baby leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Kwa sababu hiyo mwimbaji huyo aligawa chakula bure bila malipo katika mkahawa wake kwa jina Shishi Foods kati ya saa sita na saa nane mchana.
Shishi alishiriki chakula cha mchana pia na watoto yatima ambao walionekana kwenye video wakimsemea dua.
Baadaye jioni Shishi ambaye pia ni mwigizaji alitangaza kwamba kutakuwa na sherehe ya kukata keki kwenye mkahawa huo huo huku akitoa mwaliko kwa wote ambao wanaweza kufika.
Mzaliwa huyo wa wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora nchini Tanzania ametimiza umri wa miaka 35.