Mwanamume afungwa maisha kwa kuwadhulumu kimapenzi wasichana wawili

Tom Mathinji
1 Min Read

Mwanamume katika kaunti ya Machakos, amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuwadhulumu kimapenzi wasichana wawili wenye umri mdogo.

Hakimu mkuu mwandamizi wa Kithimani Khapoya, siku ya Jumanne alimhukumu kifungo cha maisha Isiah Maweu Lucas, baada ya kumpata na hatia ya kuwadhulumu kimapenzi wasichana wawili wenye umri mdogo, kinyume na sehemu ya  8(1)(2) ya sheria za makosa ya ngono.

Mahakama ilifahamishwa kwamba Maweu aliwahadaa wasichana hao wawili kutumia samakikutoka mto Athi.

Wasichana hao walinaswa na mtego wa Maweu na baadaye nyanya yao pamoja na majirani waliwapata wakiwa uchi karibu na kichaka kilicho karibu.

Kulingana na hakimu huyo, ushahidi uliotolewa na mashahidi sita, ulidhibitisha kuwa Maweu alitekeleza uovu huo kwa wasichana hao wawili.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article