Mwanamke adaiwa kumuua mpenziwe katika kaunti ya Trans Nzoia

Polisi walipashwa habari na jirani ya mwendazake, aliyesikia vurugu nje usiku wa manane na alipotoka akampata akivuja damu.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwanamke mmoja kwa jina Nancy Faiza mwenye umri wa miaka 21 anadaiwa kumuua kwa kumdunga kisu mpenzi wake kwa jina Benedict Kiptoo mwenye umri wa miaka 24 katika makazi yao eneo la Makunga, kaunti ya Trans Nzoia.

Kulingana na taarifa ya maafisa wa polisi wa kituo cha Maili Saba, ripoti kuhusu tukio hilo iliwafikia kupitia kwa Evans Letting ambaye ni jirani ya mwendazake.

Letting alisema alisikia kelele nje ya mlango wa nyumba anayoishi saa sita unusu usiku wa kuamkia leo na alipotoka nje, akampata Benedict akiwa chini huku akivuja damu.

Damu hiyo ilitokana na majeraha ya kisu yaliyodaiwa kusababishiwa na Nancy ambaye amekuwa akiishi naye.

Letting alisema alijaribu kumpa Evans huduma ya kwanza kabla ya kuanza safari kuelekea hospitalini lakini akakata roho kabla ya kufikishwa huko.

Maafisa wa polisi wa kituo cha Maili Saba pamoja na wenzao kutoka Kitale na Kwanza walifika eneo la tukio ambapo walibaini kwamba Evans na Nancy wamekuwa wakiishi pamoja kama wapenzi.

Nancy ambaye ni mshukiwa mkuu wa mauaji hayo alitoweka lakini kisu anachodaiwa kutumia kilipatikana na kuwekwa na polisi kama ushahidi.

Polisi walizuru pia chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Cherangany ambapo walibaini kwamba mwendazake alidungwa kisu mara moja tu kwenye kifua.

Mwili wake unasubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi huku mshukiwa akisakwa na polisi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *