Mwanamitandao ajiweka jela kwa siku saba

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamitandao maarufu nchini Marekani Kai Cenat alijipeleka gerezani kama mfungwa na atasalia humo kwa siku saba.

Kai ambaye amemaliza siku nne kwenye gereza hilo ambalo linasemekana kutokuwa la kweli alialika watu wengine maarufu kushirikiana nao kwenye onyesho hilo na kamera zimewekwa kila mahali.

Matukio kwenye gereza hilo yanapeperushwa mubashara mitandaoni, tukio ambalo limepatiwa jina la “7 days in”.

Wanaoshirikiana naye ni kama mwanamuziki Offset, mchekeshaji Druski na mwigizaji Teana Trump ambaye anahudumu kama askari jela. Wengi wa watu hao maarufu ni wafungwa wenza.

Wamevaa sare ambazo huvaliwa na wafungwa katika magereza kote nchini Marekani na seli zao zinafanana tu seli za kawaida.

Hata hivyo mwanamitandao huyo amekashifiwa na wengi mitandaoni. Watu wanahisi kwamba onyesho hilo halikuandaliwa kwa nia njema kwani linaonekana kufurahikia na kutukuza uhalifu na hali nzima ya kuwa mfungwa.

Share This Article