Mwanaharakati Bob Njagi apatikana hai Tigoni

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanaharakati Bob Njagi aliyetekwa nyara na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa polisi mwezi jana mtaani Kitengela, amepatikana akiwa hai katika mtaa wa Tigoni, kaunti ya Kiambu.

Kulingana ya taarifa ya Rais wa Chama cha Mawakili nchini, LSK Faith Odhiambo, Njagi ambaye alitekwa nyara Agosti 19, amepatikana akiwa ametupwa Tigoni akiwa salama.

Njagi alikamatwa na kaka wawili ambao pia wamepatikana wakiwa wametupwa mtaani Gachie wakiwa hai.

Hii inafuatia shinikizo kali kutoka kwa umma na LSK ambao waliwasilisha kesi mahakamani kumshtaki aliyekuwa kaimu Inspekta Mkuu wa Polisi Gilbert Masengeli kuhusu kutoweka kwa wanaume hao watatu.

Masengeli alikataa kufika mahakamani mara kadhaa, hali iliyosababisha yeye kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Share This Article