Msomaji wa zamani wa habari za runinga katika Shirika la Utangazaji nchini Uganda (UBC) Edward Rukidi Kijanangoma, ndiye Mfame mpya wa Tooro nchini Uganda.
Anamrithi marehemu Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi wa nne, atakayezikwa Jumamosi hii.
Mfalme Oyo, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 34, hakuwa ameoa wakati wa kifo chake kutokana na saratani na ikabidi Mfalme mpya achaguliwe kutoka kwa watu wengine wa ukoo.
Licha ya Oyo kuwa na mtoto mmoja wa kiume nje ya ndoa, kamati ya kuteua Mfalme ilikataa kumteua kuwa mrithi kwa kuwa hakuwa ametambuliwa kisheria na badala yake kumchagua Kijanangoma.
Ufalme wa Tooro ni mojawapo wa Wafalme tano za kitamaduni ambazo zinatambuliwa na serikali ya Uganda.
Hata hivyo, mamake Oyo amepinga uteuzi wa Kijanangoma huku familia hiyo ikihisi kutengwa na huenda wakaelekea mahakamani.