Mwanahabari wa KTN Shadrack Mitty afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanahabari wa runinga ya KTN Shadrach Mitty ameaga dunia Jumanne usiku, akipokea matibabu katika Hospitali ya chuo kikuu cha Kenyatta .

Kulingana na taarifa ya familia na pia mwajiri wake kampuni ya Standard Media group, Mitty aliyekuwa amefanya kazi kwa takriban mwongo mmoja aliaga dunia usiku wa manane wa Jumanne.

Mitty alikuwa mwanahabari aliyekubuhu katika masuala ya elimu .

Miongoni mwa waliomwomboleza marehemu ni mhariri wa runinga na uvumbuzi Kizito Namulanda, aliyemtaja kuwa mbunifu,makini, na aliyejituma kuifanya kazi yake.

Share This Article