Mwanahabari mkongwe Mutegi Njau amefariki

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanahabari Mkongwe Mutegi Njau ameaga dunia.

Mwanahabari mkongwe Mutegi Njau ameaga dunia. Kulingana na familia yake, Mutegi alifariki Alhamisi saa moja usiku.

“Tuna huzuni kuwafahamisha kufariki kwa baba yetu. Alipumzika kwa amani Juni 27,2024 saa moja usiku. Alikuwa mkarimu na mcheshi na licha ya kuwa msingi wa familia yetu, pia alithaminiwa sana katika jamii,” ilisema taarifa ya familia yake.

Mhariri huyo wa zamani, alikuwa akipokea matibabu katika muda wa wiki tatu zilizopita baada ya kuugua kiharusi.

Huku akiwa na tajiriba ya miaka 35 katika tasnia ya uanahabari, Mutegi alistaafu kutoka kampuni ya Nation Media Group mwaka 2005, baada ya kufanya kazi kwa muda wa miaka 24.

Kufuatia kifo chake, jamaa na marafiki wametuma jumbe za kumuomboleza mwanahabari huyo aliyewakuza wengi.

“Mutegi Njau aliwafunza wengi. ameacha mfano mwema. Ni wakati wa kupumzika,” alisema mkuu wa mawasiliano katika afisi ya Naibu wa Rais Njeri Rugeni.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *