Mwanafunzi afariki kwenye mkasa wa moto Limuru

Tom Mathinji
1 Min Read
Mtoto wa umri wa miaka 9 afariki kwenye mkasa wa moto Limuru.

Hali ya huzuni ilighubika kijiji cha Tharuni eneo la Limuru, baada ya mtoto mwenye umri wa miaka 9 kufariki kwenye ajali ya moto.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi katika shule ya upili ya Rironi, alichomeka hadi kufa wakati nyumba yao iliposhika moto.

Wakati wa tukio hilo, inaaminika kuwa wazazi wa mtoto huyo hawakuwa nyumbani, walikuwa wameondoka kuhudhuria hafla ya mazishi.

Akithibitisha kisa hicho, afisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai anayesimamia eneo la Limuru Peter Alenga, alisema uchunguzi umeanzishwa kubainisha chanzo cha mkasa huo.

Alitoa wito kwa wazazi kuwa waangalifu kuhakikisha usalama wa watoto wao hasaa wakati huu wa likizo ndefu.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article