Mwakilishi Wadi ya Chewani Hamisi Idd afariki

Tom Mathinji
1 Min Read

Hamisi Idd, ambaye ni Mwakilishi Wadi ya Chewani Kaunti ya Tana River, ameaga dunia mapema leo Jumamosi asubuhi katika ajali ya barabarani kwenye eneo la Kana-goni katika barabara kuu ya Garsen-Malindi.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini Malindi.

Idd alikuwa Mwakilishi Wadi aliyehudumu kwa kipindi kimoja ambapo alichaguliwa kwa tiketi ya chama UDA.

Kabla ya kuchaguliwa kwake, alikuwa mlinzi wa kibinafsi wa Gavana wa Tana River.

Kadhalika Idd alikuwa kiongozi wa wachache katika bunge la Kaunti ya Tana River.

Hamisi Idd, mwakilishi Wadi ya Chewani aliyefariki katika ajali ya barabarani.

Kwenye risala za rambirambi, chama cha UDA kimemtaja Idd kuwa kiongozi aliyejitolea muhanga kazini.

Katibu Mkuu wa chama cha UDA, Cleophas Malala alithibitisha kifo cha Idd akisema  wakazi wa Tana River wamepokonywa kiongozi mahiri.

“Asubuhi ya leo, tulipokea habari za kuhuzunisha kuhusu kifo cha mheshimiwa Hamisi Iddi Deye, Mwakilishi Wadi ya Chewani katika eneo bunge la Galole, kaunti ya Tana River,” alisema Malala.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *