Mvurya asisitiza umuhimu wa afya ya akili magerezani

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa Biashara na Uwekezaji nchini Salim Mvurya amesisitiza kwamba afya ya akili na ustawi wa wafanyakazi na wafungwa ni muhimu kwa mafanikio ya huduma za urekebishaji.

Akizungumza alioongoza uzinduzi wa wiki ya huduma magerezani, Mvurya alisema bila akili yenye afya, hakuwezi kuwa na utoaji wa huduma kwa ufanisi, hakutakuwa na urekebishaji wa kweli, na hakutakuwa na kuunganishwa tena katika jamii.

“Ni lazima tuzingatie mikakati inayoweza kutekelezeka ambayo itasababisha kuboreshwa kwa sera, ufikiaji bora wa huduma za afya ya akili na uundaji wa mazingira ambayo yanakuza ustawi wa jumla,” alisema Waziri huyo.

Alisema pia kwamba ni muhimu kwa viongozi kushirikiana kwa karibu na watoa huduma za afya, washirika wa maendeleo, mashirika ya kijamii au ya watu na familia.

Mvurya alisema kwamba kupitia ushirikiano, inawezekana kujenga mfumo endelevu wa usaidizi kwa afya ya akili ndani ya vituo vya kurekebisha tabia.

Alihimiza viongozi serikalini kushirikiana kuunda mfumo wa urekebishaji unaostahimili zaidi ambapo ustawi wa akili hutumika kama msingi wa kuongoza uwezo wa kukabiliana na mfadhaiko, kufanya kazi kwa ufanisi, na kudumisha mtazamo mzuri kati ya watu.

Share This Article