Mvurya aongoza mafunzo ya vyombo vya usalama kuhusu CHAN

Harambee Stars imo kundi A pamoja na DR Congo, Morocco, Angola na Zambia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa michezo Salim Mvurya leo ameongoza mafunzo ya vyombo kadhaa vya kiusalama kwa mashindano ya CHAN.

Warsha hiyo ya siku tatu inayoandaliwa katika uwanja wa Kasarani inahusu utoaji huduma za dharura na kukabiliana na mikasa katika fainali za CHAN zitakazodumu kwa mwezi mmoja.

Kenya itaandaa mechi za kundi A katika viwanja vya Nyayo na Kasarani sawia na fainali ya Agosti 30, katika uga wa Kasarani.

Harambee Stars imo kundi A pamoja na DR Congo, Morocco, Angola na Zambia.

Wenyeji wa Tanzania wataandaa mechi ya ufunguzi tarehe 2 mwezi ujao dhidi ya Burkina Faso uwanjani Mkapa.

Website |  + posts
Share This Article