Mvulana aliyemuua rafikiye aachiliwa huru Kisumu

Marion Bosire
2 Min Read

Mvulana wa umri wa miaka 10 aliyemuuwa rafiki yake wa miaka 8 katika kijiji cha Andingo kaunti ndogo ya Nyakach (Kisumu), ameachiliwa huru na mahakama ya Kisumu.

Mvulana huyo aliyesajiliwa kama N.A.S, alidaiwa kumuuwa T.D.O.tarehe 25 Nov.2023 na kufikishwa mahakamani tarehe 8 Aprili 2024 ila mwendesha mashtaka akaomba muda zaidi kubaini umri kamili wa N.A.S kabla kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Mei 21, 2024 alifanyiwa uchunguzi wa kiakili na kupatikana kuwa timamu.

Licha ya uhakika huo, upande wa N.A.S ulidai kuwa kifungu cha nne cha mwaka wa 2022 hakiruhusu mtu wa chini ya umri wa miaka 12 kushtakiwa kwa kosa la mauji kwa kigezo kuwa hajielewi hivyo ukaomba apelekwe kwenye kituo cha maslahi ya watoto.

Kauli hiyo ilipingwa na mwendesha mashtaka James Marete aliyedai kuwa kifungu cha 221 cha sheria za watoto ya mwaka wa 2022 inatoa fursa ya kudhibitisha au kukataa hivyo ni vyema mshukiwa afikishwe kizimbani ili kifungu cha miaka kisitumike vibaya. Aliongeza kuwa ni bora kwa mahakama kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka ili kubaini iwapo mshukiwa alifahamu zuri na baya wakati wa tukio.

Hata hivyo, Jaji Roselyne Aburili alikumbatia tetesi za upande wa N.A.S. kwa hoja kuwa sheria hairuhusu mtu wa umri wa mshukiwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji kwa sababu angali na mawazo changa. Aliagiza N.A.S. apelekwe kwa kituo cha maslahi ya watoto kwa ajili ya malezi mema

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *