Mvua ambayo inashuhudiwa katika sehemu tofauti za nchi, itaendelea kunyesha juma hili, kulingana na Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa.
Kulingana na utabiri wa idara hiyo wa siku 7, mvua itashuhudiwa katika sehemu za nyanda za juu mashariki na magharibi mwa Rift Valley, eneo la ziwa Victoria, eneo la bonde la ufa, ukanda wa pwani, Nyanda za chini kusini mwa nchi na kaskazini mashariki.
Utabiri huo ulidokeza kuwa viwango vya joto nyakati za mchana vya zaidi ya nyuzijoto 30 vitashuhudiwa katika mwambao wa pwani, Kaskazini Mashariki na Kaskazini Magharibi mwa nchi.
Viwango vya joto nyakati za usiku vinatarajiwa kuwa chini ya nyuzi joto 10 katika maeneo ya nyanda za juu mashariki na magharibi mwa Rift Vally, eneo la kati mwa bonde la ufa na pembezoni mwa mlima Kilimanjaro.