Gazeti moja nchini Algeria limekiri kuhusika kwa Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE katika mapinduzi ya serikali nchini Niger.
Gazeti hilo la lugha ya Kifaransa lijulikanalo kama Le Soir d’Algerie, limetoa taarifa kuwa UAE ulihusika katika mapinduzi ya serikali ya Rais Mohamed Bazoum.
Yamkini Balozi wa Niger mjini Abu Dhabi ambaye zamani alikuwa mkuu wa majeshi alisaidiwa na serikali ya UAE kufanikisha mapinduzi hayo.