Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, umewafurusha baadhi ya viongozi wake, kwa madai kwamba wameteuliwa serikalini au wanashirikiana na vyama au miungano hasimu ya kisiasa.
Ktaarifa siku ya Jumatatu, baadhi ya wale waliofurushwa ni pamoja na Mawaziri Hassan Joho (Madini), Wycliffe Oparanya (Vyama vya Ushirika), James Opiyo Wandanyi (Nishati), Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na mbunge mteule Sabina Chege.
Wengine waliotimuliwa ni Abdi Noor Farah, wabunge Adan Keynan (Eldas), David Pkosing (Pokot Kusini), Mishi Mboko (Likoni), Abdul Haji (Samburu Magharibi), Isabella Githinji, Caroline Karugu, na Solomon Kuria.
Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kuandiliwa kwa mkutano wa Baraza Kuu na Baraza Tekelezi la Kitaifa la muungano huo siku ya Jumatatu.
Wakati huo huo, muungano huo umemteua Caroli Omondi kuwa kiongozi wake bungeni na hivyo kutamatisha hatamu ya Junet Mohammed kwenye wadhifa huo.
Umesema hivi karibuni utatangaza orodha ya viongozi watakaochukua nyadhifa zilizoachwa wazi.