Umoja wa Afrika washutumu jaribio la mapinduzi Niger

Dismas Otuke
1 Min Read

Umoja wa Afrika, AU umeshutumu jaribio la mapinduzi ya serikali nchini Niger.

Baadhi ya walinzi wa Rais Mohamed Bazoum walimgeuka, kumfungia na kumzuia kuondoka katika kasri lake mjini Niamey.

Hata wafanyakazi wa ikulu walizuiliwa kutoka nje.

Hali hiyo ilisababisha makabiliano makali kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono Rais na wale wanaompinga na kuchangia kujeruhiwa kwa mtu mmoja.

Mwenyekiti wa AU Musa Faki ameshutumu jaribio hilo akisema ni usaliti mkubwa kwa raia wa Niger na kutaka wahusika kusitisha vitendo hivyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *