Muturi: Utoaji hudumua katika utumishi wa umma utaimarishwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Moses Kuria (Kushoto) amkabidhi justin Muturi wizara ya utumishi wa umma.

Waziri mpya wa utumishi wa umma Justin Muturi, ameelezea kujitolea kwake kuimarisha utoaji huduma na uwajibikaji katika sekta ya utumishi wa umma.

Alipokuwa akikabidhiwa rasmi wizara hiyo iliyoshikiliwa awali na Moses Kuria, Muturi alisisitiza haja ya kuendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, kuhakikisha taifa hili linazidi kupiga hatua.

“Tunahitaji kuendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, ili taifa hili lisonge mbele,” alisema Muturi.

Waziri huyo aliangazia magaeuzi yanayoendelea katika utumishi wa umma, akihakikisha kuwa mageuzi hayo hayapaswi kuashiria kuwa kuna watu wanalengwa au afisi.

“Ipo haja ya kuendelea kutathmini jinsi tunavyowahudumia wananchi, hatua hii hailengi mtu yeyote au afisi wanazoshukilia,” alisema Muturi.

Alisema atasikiliza maoni na mawazo yanayolenga kuimarisha utoaji huduma, huku akisifu hatua kubwa zilizopigwa na mtangulizi wake Moses Kuria.

“Niko tayari kusikiliza maoni ya kuimarisha utoaji huduma. Nampongeza Moses Kuria kutokana na hatua kubwa alizopiga katika kipindi cha muda mfupi aliposhikilia afisi hiyo,” alisema Muturi.

Awali Muturi alikuwa mwanasheria mkuu, kabla ya kuteuliwa na Rais William Ruto kuwa waziri wa Utumishi wa umma.

Website |  + posts
Share This Article