Museveni aonyeshwa kivumbi uchaguzi mdogo wa Kawempe

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama tawala nchini Uganda, National Resistance Movement (NRM), chake Rais Yoweri Museveni, kimeonyeshwa vumbi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kawempe kaskazini.

Hii ni baada ya Elias  Luyimbazi Nalukoola wa chama National Unity Platform (NUP)  kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo mdogo ulioandalwia jana.

Nalukoola alipata kura 17,764 akifuatwa na Fariba Nambi wa chama cha NRM kwa kura 8,593.

Chama cha NUP kinaongozwa na mbunge wa zamani ambaye pia msanii Bobi Wine.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *