Museveni aagana na Balozi wa Urusi Semivolos

KBC Digital News
1 Min Read
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni (kulia) na Balozi wa Urusi Vladlen Semivolos

Rais Yoweri Kaguta Museveni ameaga Balozi wa Urusi anayemaliza muda wake nchini Uganda Vladlen Semivolos katika Ikulu ya Entebbe.

Katika mazungumzo yao, Rais Museveni na mgeni wake walikumbuka historia ya uhusiano kati ya Uganda na Urusi na kusifu mchango wake mkubwa katika kuimarisha na kustawisha mahusiano hayo ya pande mbili.

Rais Museveni alimtakia Balozi Semivolos heri anapoanza hatua mpya ya maisha yake.

“Nakupongeza kwa kukamilisha majukumu yako hapa, na natambua juhudi zako za kulinda ukaribu na ushirikiano uliopo kati ya mataifa na wananchi wetu. Nakutakia mafanikio mema katika mipango yako ya baadaye,” akasema Rais Museveni.

Kwa upande wake, Semivolos alishukuru kwa mapokezi ya ukarimu na urafiki alioupata wakati wa kuhudumu kwake nchini Uganda.

“Najivunia na ninaona kuwa ni heshima kubwa kupata nafasi ya kuhudumu Uganda, na ninathamini sana ushirikiano wenu katika nyanja mbalimbali ambao umeleta manufaa kwa Uganda na Urusi,” akaongeza.

Share This Article