Waziri wa masuala ya vijana ,uchumi bunifu na michezo Kipchumba Murkomen, ameandaa kikao ha kutathmini utendakazi na kujadili mustakabali wa wizara hiyo.
Akihutubu Murkomen amesema utathmini sio tu kuangazia ufanisi, bali pia changamoto na mapungufu ili kusaidia kusonga mbele.
Waziri alisema haya Juamatano kwenye kikao cha kutathmini utendakazi na kuweka malengo ya mwaka 2024 na 2025, akiwa na katibu wa baraza la mawaziri Mercy Wanjau na naibu mkuu wa utumishi wa umma Eliud Owalo.
“Huu mchakato unatuwezesha kujiwianisha na mipango mipana ya serikali kuhakiksha matakwa ya Wakenya yameangaziwa.
Murkomen aliandamana na makatibu wake akiwemo yule wa maswala ya vijana Maalim Ismail na mwenzake wa michezo Peter Tum.