Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, ameagiza kupandishwa vyeo kwa Machifu walio na shahada za digrii hadi kuwa manaibu Makamishna wa kaunti.
Murkomen ameongeza kuwa kila kata ndogo yapaswa kuwa na Machifu wawili ili kuimarisha utendakazi.
Waziri alisema haya jana katika kaunti ya Tana River, akiwa kwa ziara ya eneo hilo kutathmini hali ya kiusalama.
Kulingana na Murkomen, kupandishwa vyeo kwa Machifu walio na digrii kutawamotisha na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.