Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, amewahimiza viongozi wa Lamu kudumisha amani na usalama katika Kaunti hiyo ili kufanikisha maendeleo.
Mudavadi alisema hakuna Kaunti inayoweza kuvutia uwekezaji na nafasi za ajira iwapo haina utulivu na umoja wa kimaendeleo.
Mudavadi alisema serikali kuu itaendelea kuwekeza katika usalama wa Lamu na Kaunti nyinginezo za Pwani, akitaja kuwa vizazi katika Kaunti hiyo na kwingineko, vimefadhaika kutokana na kuzorota kwa usalama.
Waziri Mudavadi, yuko katika ziara ya siku tatu katika kaunti ya Lamu, ambako alikutana na viongozi waliochaguliwa kwenye Kaunti hiyo wakiongozwa na Gavana Issa Timamy.
Aidha, alikagua ujenzi wa jukwaa la kusubiria la halmashauri ya Bandari ya humu nchini katika eneo la Mokowe.