Mudavadi: Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na China umeimarika

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, amesema kuna haja ya Kenya na China kutumia vyema fursa ya kukuza ushirikiano wao wa kimkakati hadi ngazi za juu.

Musalia ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje,  amesema nchi hizo mbili zinahitaji kukumbatia ushirikiano unaozingatia uadilifu na maendeleo ambayo yanakidhi matakwa ya kizazi cha sasa.

Alitoa wito wa kuwekwa mustakabali endelevu kati ya Kenya na China,  ili kuafikia malengo ambayo zinataka.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya kuadhimisha miaka 60 ya urafiki baina ya mataifa haya mawili, waziri huyo alitambua kuwepo kwa tofauti miongoni mwa nchi hizi mbili, lakini akasisitiza matarajio yao ya pamoja ya maendeleo ya haraka ya kuafika upeo mkubwa wa kimaisha na kiviwanda.

Alipongeza nchi ya China kwa miradi yake ya maendeleo iliyoko Kenya na Afrika kwa ujumla, akisema kuwa ushirikiano wa kina wa kimkakati kati ya mataifa haya mawili, umechangia matokeo bora katika sekta za kijamii na kiuchumi nchini.

Share This Article