Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, ametoa wito kwa mashirika ya serikali kushirikiana katika kufanikisha miradi ya serikali.
Kulimgana na waziri huyo wa mambo ya nje, raslimali nyingi kutoka kwa wafadhili na washirika wa kimaendeleo, zinatumiwa vibaya.
Mudavadi alisikitikia matumizi mabaya ya rasli-mali muhimu kutokana na ukosefu wa ushirikiano, akisema hali hiyo imesababisha serikali kushindwa kutekeleza miradi muhimu ya maendeleo.
Alielezea haja ya juhudi za pamoja katika kutumia vyema rasilimali zilizopo, akidokeza kuwa wakenya wanatarajia kupata huduma bora ambazo zitabadilisha maisha yao.
Akizungumza leo Alhamisi alipoongoza mkutano wa washirika wa kimaendeleo afisini mwake, Mudavadi alisema atahakikisha mashirika ya serikali chini ya afisi yake, yanatatua changamoto zinazokabili utoaji huduma serikalini.