Mudavadi: Maafisa wa serikali wanafaa kuchukulia shughuli za bunge kwa uzito

Martin Mwanje
1 Min Read
Musalia Mudavadi - Mkuu wa Mawaziri

Maafisa wa serikali wametakiwa kuchukulia shughuli za bunge kwa uzito unaostahili kwa kuwaandalia mawaziri majibu madhubuti na yaliyotafitiwa vyema wakati wa kujibu maswali bungeni. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Mkakati wa 2023-2027 wa Idara ya Masuala ya Bunge.

Mudavadi amesema majibu bayana na ya kweli siyo tu kwamba yanaonyesha dhamira ya serikali ya kuboresha maisha ya Wakenya bali pia yanaongeza imani ya umma katika uongozi wa nchi,

“Kushindwa kujibu maswali ipasavyo bungeni huharibia taswira ya serikali na kuwaacha Wakenya wakihisi kutosikizwa.” alisema Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje.

“Visa vingi vya Wakenya kufadhaika vinatokana na ukosefu wa kuelezea bayana hatua zinazochukuliwa na serikali. Ikiwa maafisa wa serikali hawawezi wakatoa majibu kwa njia ya ufasaha bungeni, wanawezaje kuwa na matumaini ya kuangazia masuala yaliyoibuliwa na Wakenya?”

Kadhalika, Mudavadi amewataka watumishi wa umma wanaojihusisha na sera na uundaji wa sheria kutekeleza majukumu yao kwa uzalendo, uadilifu na kwa njia bora.

tion to act with patriotism, integrity, and efficiency.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *