Mudavadi: Kilimo huchangia kwa uthabiti wa taifa hili

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesema kilimo ni muhimu sana,kwa kuwa husababisha uthabiti wa taifa hili.

Akizungumza Alhamisi alipofunga kongamano la kila mwaka kuhusu kilimo biashara, waziri huyo wa Mambo ya Nje alisema kilimo kinasalia kuwa nguzo kuu kwa ajenda ya maendeleo ya taifa hili.

“Kilimo ni kichocheo kikuu cha uchumi wa mashinani, utoshelevu wa lishe bora, na msingi ambao hutegemewa na mamilioni ya familia,” alisema Mudavadi.

Alitoa wito wa kuibadili sekta ya kilimo kuwa yenye ushindani, inayotumia teknolojia ya kisasa ili isaidie kufanikisha mageuzi ya taifa hili.

Mudavdai said the summit stands as a powerful platform to reposition agriculture as a competitive, profitable, and technology-driven enterprise that fuels Kenya’s economic transformation.

Aidha, waziri huyo alidokeza kuwa serikali imeimarisha mfumo wa uzalishaji, ufanisi wa masoko na kuhakikisha miundombinu ya kisasa katika maeneo ya mashinani ili kupiga jeki sekta nzima ya kilimo.

“Mikakati hii inawiainisha shughuli za kaunti na za kitaifa, kupunguza utumizi mbaya, kuhakikisha masoko ni thabiti na kutoa matokeo bora kwa wakulima na wajasiriamali,” aliongeza waziri huyo.

Kongamano hilo la mwaka huu liliwaleta pamoja viongozi wa serikali, wale wa sekta ya kibinafsi, wasomi, washirika wa kimaendeleo, kwa lengo la kufanyia mabadiliko sekta ya kilimo.

Website |  + posts
Share This Article