Mudavadi: Utafiti ni muhimu kwa maendeleo ya taifa

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi ametoa wito kwa Wakenya kukumbatia utafiti wa elimu na teknolijia ili kuhakikisha maendeleo ya taifa.

Akizungumza alipofungua kongamano la AISC katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Mudavadi alisema kupitia utafiti na ushirikishanaji wa habari, Kenya inaweza kubuni uwezo wa kushugulikia changamoto zinazokumba taifa hili na ulimwengu kwa jumla.

Alihimiza umma kukumbatia teknolojia na fursa za kidijitali zilizopo kujiendeleza.

Kongamano hilo linalenga kusisitiza haja ya kutunza mazingira katika juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Hii inatoa wito wa uhifadhi sio tu kupitia mwongozo wa usawa lakini pia kupitia mipango ya maendeleo,” alisema Mudavadi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *