Mudavadi atoa wito wa kukabiliana na ueneaji wa silaha ndogo

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu aliye pia kaimu waziri wa usalama wa taifa Musalia Mudavadi, ametoa wito wa juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto inayotokana na ueneaji silaha ndogo katika eneo la Maziwa Makuu na Upembe wa Afrika.

Mkutano huo ulioandaliwa Jijini Nairobi, uliwaleta pamoja maafisa wa kuu wa polisi na makatibu wa wizara za usalama kutoka mataifa wanachama wa kituo cha kanda kuhusu silaha ndogo, (RECSA).

Katika mkutano huo, Mudavadi alisema kuwa hali ya kutodhibitiwa kwa ueneaji wa silaha ndogo, imeendelea kuchochea mizozo ya kijamii, matumizi haramu ya maliasili na ugaidi miongoni mwa aina nyingine za uhalifu.

Mudavadi alitoa wito kwa mataifa wanachama wa RECSA, kuimarisha uwezo wa kushughulikia changamoto za kiusalama kikamilifu.

Alielezea masikitiko yake kwamba hali hiyo inatatiza amani, usalama na ustawi katika eneo hilo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *