Mtihani wa kitaifa nchini Uganda, UCE ulioanza Jumatatu kwa somo la Hisabati umeingia siku ya nne leo Alhamisi chini ya mtaala mpya wa elimu.
Jumla ya watahiniwa 379,620 wanakalia mtihani huo wakiwa ni pamoja na 369,477 chini ya mtaala mpya na 10,143 wakikalia mtihani wa mtaala wa zamani.
Leo wanafunzi wanaanza kwa somo la Kemia ya vitendo, kabla ya kufanya Kemia ya nadharia na hatimaye kumaliza kwa Insha ya Kimombo jioni.
Mfumo wa elimu nchini Uganda hujumuisha miaka 7 ya shule ya msingi, 6 ya shule ya sekondari na 3-5 ya vyuoni.