Mtangazaji mkongwe wa VOA, Shaka Ssali, afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Mtangazaji mkongwe wa shirika la utangazaji nchini Marekani, VOA, Shaka Ssali, ameaga dunia jana Alhamisi akiwa na umri wa miaka 71.

Ssali alipata umaarufu kwa kuongoza kipindi cha “Straight Talk Africa” kwa zaidi ya miaka 20 alipowahoji viongozi mbalimbali.

Ssali ambaye alikuwa aadhimishe umri wa miaka 72 tangu kuzaliwa kwake katika kipindi cha wiki mbili zijazo, alifariki akiwa eneo la Virginia, Marekani.

Mtangazaji huyo nakumbukwa kwa mchango wake maridhawa katika tasnia ya utangazaji, na pia alikuwa mmoja wa waanzilishi wa wakfu wa “The Ford Foundation.”

Mwanahabari huyo alizaliwa nchini Uganda; kabla ya kuhamia Marekani, alikofanikiwa kujiunga na VOA na kutangaza kwa miaka 29, akistaafu mwaka 2021.

Ssali pia aliwahi kutunukiwa tuzo ya maisha na VOA, na tuzo nyingine ya serikali ya Uganda kwa raia wake walio ughaibuni.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *