Mtandao wa KFC wasemekana kudukuliwa

Marion Bosire
1 Min Read

Video inayosambaa mitandaoni inaashiria uwezekano wa kudukuliwa kwa mtandao wa duka la chakula la KFC. Katika video hiyo, viwambo vilivyopachikwa dukani ambavyo mara nyingi huwa na maonyesho ya vyakula vinaonekana vikipitisha maneno ya kutangaza udukuzi huo.

Maneno “Hacked by Mutaarif Hamas Islamic Force” yaani “imedukuliwa na jeshi la kiisilamu la Mutaarif Hamas” yanaonekana yakipita kwenye viwambo hivyo kulingana na video hiyo.

Inaripotiwa kwamba viwambo vya KFC vipatavyo 200 vilidukuliwa katika maeneo mbali mbali ulimwenguni na haijulikani ilikorekodiwa video hiyo.

Usimamizi wa duka hilo la chakula KFC haujatoa taarifa kuhusu tukio hilo.

Tutakufahamisha mengi kuhusu taarifa hii pindi yatakapochipuka.

Share This Article