Mswada wa Fedha wa mwaka 2023 waidhinishwa

Tom Mathinji
1 Min Read

Wabunge Jumatano jioni walipiga kura kuidhinisha mswada wa fedha wa mwaka 2023.

Mswada huo ulipitishwa baada ya kuungwa mkono na wabunge 176 huku wabunge 81 wakiupinga.

Jumla ya wabunge 257 walipiga kura. Kura hiyo ilipigwa baada ya mjadala mkali uliodumu mchana kutwa.

Baadhi ya mapendekezo kwenye mswada huo ambao wakenya wanaochukulia kuwa yasiyowafaa yalipingwa.

Baadhi ya ada zilizopendekezwa zilirekebishwa huku nyingine zikisalia vivyo hivyo.

Siku ya Jumanne, kamati ya bunge la taifa kuhusu fedha na mipango ya kitaifa, iliwasilisha mswada wa fedha wa mwaka huu uliofanyiwa marekebisho baada ya wananchi kutoa maoni yao kuhusu mswada huo.

Mswada huo sasa utawasilishwa kwa kamati ya bunge lote ambalo litatathmini marekebisho ya wabunge katika shughuli itakayotekelezwa juma lijalo.

Website |  + posts
Share This Article