Mshukiwa wa wizi akamatwa Tigoni

Jamaa huyo kwa jina Alex Mbugua Chege anahusishwa na wizi wa kimabavu na ubakaji wa kundi katika eneo la Tigoni.

Marion Bosire
1 Min Read

Maafisa wa upelelezi kutoka makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, DCI, wamemkamata mshukiwa mmoja anayehusishwa na matukio kadha ya uhalifu.

Jamaa huyo kwa jina Alex Mbugua Chege anahusishwa na wizi wa kimabavu na ubakaji wa kundi katika eneo la Tigoni, huku msako wa kuwakamata washirika wake ukiimarishwa.

Mshukiwa Alex alikamatwa kufuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na maafisa wa upelelezi.

Uchunguzi zaidi umebaini kwamba genge lililohusika na mashambulizi hayo ya kutisha linaundwa na wahalifu waliotoroka kutoka Kituo cha Polisi cha Limuru mnamo Novemba 4, 2026.

Operesheni hiyo inayoongozwa na maafisa kutoka Kitengo cha Utafiti wa Uhalifu na Ujasusi pamoja na Kikosi cha Operesheni Maalum inaendelea, huku maafisa hao wakiwafuatilia kwa karibu washukiwa wengine ambao bado hawajakamatwa.

Share This Article