Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati akamatwa Migori

Martin Mwanje
1 Min Read
Calvin Okoth Otieno - Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kamagambo, kaunti ya Migori wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati na kunasa misokoto 401 ya bangi.

Mshukiwa huyo alimakatwa baada ya raia kupiga ripoti kwa maafisa wa polisi juu ya gari la usafiri wa umma, nambari ya usajili, KDM 981Z, walilolitilia shaka.

 

Gari hilo lilikuwa safarini kuelekea Kisumu kutoka Migori, likiwa limepakiwa mizigo iliyokuwa na bangi hiyo.

Upekuzi uliofanyiwa gari hilo ulifichua kuwepo kwa mabegi mawili yaliyokuwa na jumla ya misokoto 401 ya bangi yenye uzito wa kilo 34.4.

Thamani ya bangi hiyo ilikadiriwa kuwa shilingi milioni moja.

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI inasema wakati wa kukamatwa kwake, dereva wa gari hilo aliyetambuliwa kama Calvin Okoth Otieno, alikuwa amebeba wanafunzi pekee, kwa kudhania wanafunzi hao wangekuwa kinga dhidi ya yeye kutiliwa shaka.

Okoth kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kamagambo akisuburi kufikishwa mahakamani.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *