Mshukiwa wa ugaidi ahukumiwa miaka 30 gerezani

Tom Mathinji
1 Min Read

Mahakama moja ya Busia imemhukumu mshukiwa wa ugaidi miaka 30 gerezani, baada ya kukamilika kwa kesi iliyoanza kusikilizwa mwaka 2021.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, DCI, Jackton Jacob Kanoti almaarufu Abdul Hakim, alitiwa nguvuni katika kaunti ya Siaya kwa madai ya kuhusika katika vitendo vya ugaidi vya kundi la Al-Shabaab na lile la  wanamgambo la Islamic State nchini Iraq.

Kupitia ukurasa wa X, DCI ilisema wakati wa kutiwa nguvuni,  Kanoti alipatikana na vifaa vinavyohusishwa na shughuli za kigaidi pamoja na rununu aliyoitumia kupokea habari za kigaidi kupitia video.

Katika kutoa hukumu hiyo, mahakama ilisema ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ni wa kuaminika na hivyo ikamhukumu mshukiwa miaka 30 gerezani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *