Mshukiwa wa mihadarati anaswa Kisauni

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa Polisi kutoka idara ya kukabiliana na mihadarati Kisauni wamemnasa mshukiwa mmoja wa ulanguzi wa dawa za kulevya katika eneo la Bakarani, kaunti ndogo ya Kisauni.

Mwnaume Bakarani,Mwanaume huyo aliye na umri wa miaka 45 ,Abdalla Said Omar  alikamatwa  alikamatwa kwenye makao yake huku polisi walipata pia gramu 300 za dawa za kulevya aina ya Heroin iliyofichwa ndani ya mifuko ya kijani na nyekundu.

Pia polisi walipata mashine mbili za kupima uzani.

Mshukiwa amewekwa kwenye kituo cha polisi cha Mjambere huku uchunguzi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.

Website |  + posts
Share This Article