Mshukiwa wa jaribio la mauaji ajisalimisha kwa polisi

radiotaifa
1 Min Read

Mshukiwa wa jaribio la mauaji Elias Mutugi, ambaye ni kasisi anayedaiwa kumdunga kisu mkewe kaunti ya Nakuru, amejisalimisha kwa polisi leo Jumatatu.

Huduma ya taifa ya polisi kupitia mtandao wa X, ilisema Mutugi alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Menengai akiwa ameandamana na wakili wake.

“Leo Novemba 25, 2024 Elias Mutugi Njeru mshukiwa wa jaribio la mauaji dhidi ya Florence Wanjiku Gichohi….alijiwasilisha katika kituo cha polisi cha Nakuru, akiwa ameandamana na wakili wake  Gakuhi Chege and Associates Advocates,” ilisema huduma ya taifa ya polisi.

Hatua ya kukamatwa kwake imejiri baada kusakwa na polisi kwa kujaribu kumuua mpenziwe kwa kumdunga kisu na kumsababishia majeraha makubwa.

Amekuwa mafichoni tangu Alhamisi iliyopita alipodaiwa kutekeleza uhalifu huo nyumbani kwao eneo la Kiamunyi, Rongai kaunti ya Nakuru.

TAGGED:
Share This Article