Msemaji wa zamani wa polisi ateuliwa kamanda wa Rift Valley

Marion Bosire
1 Min Read
Inspekta Jenerali Japhet Koome

Jasper Ombati ambaye aliwahi kuhudumu kama msemaji wa polisi, ameteuliwa kuwa kamanda wa polisi katika eneo la Rift Valley katika mabadiliko yaliyotangazwa Ijumaa.

Kulingana na mabadiliko hayo yaliyotekelezwa na inspekta jenerali Japhet Koome, Ombati anachukua mahali pa Tom Odero ambaye amekuwa akihudumu tangu Machi, 2023.

Odero amerejeshwa katika makao makuu ya polisi jijini Nairobi.

Ombati alikuwa amekwenda kuhudumu kama mshauri kwenye afisi ya umoja wa mataifa ya Italia na alirejea Februari mwaka huu na kufanywa kamanda wa polisi wa reli na bandari.

Wadhifa wake katika kitengo hicho cha bandari na reli sasa unashikiliwa na Allan Sangoro ambaye pia amerejea hivi maajuzi kutoka kwa afisi ya Umoja wa Mataifa ya Ethiopia.

Ombati ametumwa katika eneo la bonde la ufa wakati ambapo oparesheni kali inaendelea ya kutokomeza wezi wa mifugo na majambazi. Tajriba yake katika nyadhifa mbali mbali kikosini huenda ikamsaidia kurejesha utulivu katika eneo hilo.

Website |  + posts
Share This Article